Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tuchel aeleza mipango yao kwa Haaland

Haaland Pic Data Mshambuliaji anaewindwa na vilabu vingi kwa sasa,

Fri, 22 Oct 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha wa Klabu ya Chelsea, Mjerumani Thomas Tuchel, amefunguka namna ambavyo wanafanya mijadala ya kumsaini mpasia nyavu wa Dortmund Erling Haaland, na kuna matamanio ya kumuona akicheza katika viunga vya Klabu hiyo.

Haaland amekuwa akiwaniwa na klabu kadhaa, Ulaya baada ya kuwa na kiwango cha kuvutia kule Dortmund akifunga mabao 41 katika mechi 41 alizocheza, kwenye mashindano yote msimu huu.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21, amefunga mabao 70 katika mechi 69 kwa klabu hiyo ya Ujerumani tangu alipohamia hapo Januari 2020 , ni mshambuliaji wa Bayern Munich pekee, Robert Lewandowski (mabao 88 katika mechi 73), ambaye ana mabao mengi zaidi kushinda yeye.

Mkataba wake wa sasa amebakiza miaka miwili na nusu pale kwenye dimba la Signal Iduna Park na Dortmund hawana presha kumuuza straika wake huyo, baada ya kumtoa Jadon Sancho aliyetua Manchester United kwa pauni milioni 72.9.

Hata hivyo, kipengele cha kununuliwa kwa Euro milioni 75 kinafikia mwishoni mwa msimu huu na Tuchel ameonyesha ishara kuwa, Chelsea inaweza kukamilisha usajili wa straika huyo.

"Tulizungumza kuhusu Erling Haaland mara nyingi tu, ukiwamo wakati wa dirisha la uhamisho," amesema Tuchel akiiambia Sport Bild.

"Bado tunazungumza kuhusu yeye mara kwa mara, bilashaka kwa sababu yeye ni mchezaji muhimu na ni wazi kwamba tunamhitaji."

Chanzo: www.tanzaniaweb.live