Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tuchel: Man City ndio timu bora barani Ulaya kwa sasa

T. Tuchel Gg.jpeg Kocha wa Bayern Munich, Thomas Tuchel

Tue, 11 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Thomas Tuchel amesema kuwa timu ya Manchester City inayonolewa na Pep Guardiola inatoa kiwango cha juu zaidi cha soka barani Ulaya.

Timu hiyo ya Bavaria itasafiri hadi Uwanja wa Etihad siku ya leo kumenyana na City walio katika hali nzuri katika mechi ya kwanza ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa.

Vijana hao wa Guardiola wameshinda mechi zao saba za mwisho katika michuano yote na kuwaacha mashabiki wao wakiwa na ndoto ya kutwaa mataji matatu wakifukuzana na vinara wa Ligi Arsenal, huku wakiwa wamefika hatua za mwisho za Ligi ya Mabingwa na Kombe la FA.

Mechi ya leo itakuwa mechi ya nne kwa Tuchel kuinoa Bayern tangu achukue nafasi ya Julian Nagelsmann aliyetimuliwa.

Tuchel alisifu ushawishi wa Guardiola kwa City na kuwaweka kama moja ya timu bora zaidi barani Ulaya, ingawa pia anahisi hiyo inafanya fursa ya kuwatupa nje ya Uropa kuwa ya kuvutia zaidi baada ya kuwafunga Citizen kwenye fainali ya 2020-21 wakati akiwa kocha wa Chelsea.

Tuchel amesema; “Nadhani unaweza kuona wazi kwamba kuna miaka sita au saba ya Pep katika timu hii, anakera sana akiwa na bila mpira, akiwa na shinikizo la hali ya juu. Nadhani Pep anathibitisha kila mahali kwamba anazipa timu zake mguso wake mwenyewe”

City inaongozwa na mshambuliaji Erling Haaland, ambaye amefunga mabao 44 katika michuano yote msimu huu katika kampeni yake ya kwanza tu nchini Uingereza tangu ajiunge nayo akitokea Borussia Dortmund.

Tuchel anahofia ubora wa Haaland, na washambuliaji wengine wa City ambao wanaweza kuwepo hii leo. Beki Matthijs de Ligt atakuwa mmoja wa wale waliopewa jukumu la kujaribu kunyamazisha Haaland huko Etihad, na anahisi itahitaji juhudi kamili ya timu kufanya hivyo.

Bayern watakuwa bila mshambuliaji wao mmoja kutokana na tatizo la goti kumaanisha kuwa Eric Maxim Choupo-Moting, ambaye amefunga mabao manne ya Ligi ya Mabingwa msimu huu, hatakuwepo.

Serge Gnabry anaweza kuwa mchezaji ambaye Tuchel atamchagua kucheza mbele, huku Kocha huyo mwenye umri wa miaka 49 akieleza hadhani kama kuna kitu kibaya kwa Serge kucheza kwenye namba tisa katika mchezo wa leo kwani ana ubora unaostahili.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live