Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tuchel, Emery uso kwa uso Uefa super Cup

Uefa Super Cup.jpeg Mechi ya fainali Uefa Super Cup

Wed, 11 Aug 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ni vita ya Dakika 90' kati ya mabingwa wa Ligi ya Mabingwa barani Ulaya, Klabu ya Chelsea kutoka nchini England dhidi ya Mbingwa wa Kombe la Uropa, Klabu ya Villareal kutoka nchini Hispania.

Mchezo huo utapigwa leo Agosti 11,2021 majira ya saa nne Usiku (4:00), huko katika dimba la Windsor Park Ireland ya Kaskazini.

Klabu ya Chelsea inapewa nafasi kubwa ya kuibuka mshindi katika mchezo huo, japokua vijana wa Unai Emery wamejiandaa vya kutosha ili wapate kuwashangaza wababe hao wa Epl.

Fainali ya Uefa Super Cup huwakutanisha mabingwa wa Ligi ya Mabingwa barani Ulaya na Bingwa wa Kombe la Uropa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live