Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tuanze kuwalinda kina Kayoko, Mwandembwa

Kayoko Pic Data Mwamuzi Ramadhan Kayoko

Sat, 9 Mar 2024 Chanzo: Mwanaspoti

JUZI Rais wa TFF, Wallace Karia alifanya ziara ya kiofisi katika makao makuu ya gazeti hili hapa Tabata Relini na alizungumza masuala mbalimbali.

Mojawapo kati ya aliyozungumza ni kutopata fursa kwa marefa wa Tanzania katika mashindano makubwa ya soka duniani kama vile fainali za Mataifa ya Afrika (Afcon) na zile za Kombe la Dunia.

Karia amewatetea na kusema ana imani kubwa na marefa wa Kitanzania na mwenendo wao wa uchezeshaji unamridhisha yeye na shirikisho lake japo kuna changamoto za hapa na pale ambazo huwa hazikosekanagi.

Akasema hata vigogo wa Fifa na CAF wamekuwa wakimshangaa na kumwambia Tanzania tumekuwa tunashindwa kuwalinda marefa wetu kwa kuwafungia mara kwa mara pindi wanapofanya makosa, pia tumekuwa tunawasema vibaya sana.

Hivyo ametoa wito tuanze kuwalinda ili tusiwaharibie ulaji wao huko kwenye mashirikisho makubwa ya soka jambo ambalo litakuwa na manufaa kwao na kwetu kama nchi tofauti na hali ilivyo hivi sasa.

Ushauri wa Karia ni mzuri, pia haupaswi kutumika vibaya na marefa kwa kufanya makosa ya makusudi kisa tu wanafahamu fika sasa wana kinga na ulinzi kutoka TFF na wadau wa soka nchini jambo ambalo litakuwa linabomoa badala ya kujenga.

Wanapaswa kujiandaa vyema kabla ya mechi na wajitahidi kuchezesha vizuri ili washawishi watu wawape huo ulinzi badala ya kufanya makosa mengi ambayo mwisho wa siku yatafanya kusiwe kunapatikana matokeo ya haki katika mechi mbalimbali.

Wakumbuke haki zinaenda sambamba na wajibu wakati wao wanapolindwa basi nao wanapaswa kuzilinda timu kwa kutafsiri vyema sheria za mchezo wa mpira wa miguu pindi wanapokuwa katika utekelezaji wa majukumu yao.

Chanzo: Mwanaspoti