Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tuache siasa za wazawa, tujikite kwenye tatizo la msingi

Mzize MAYELE Tuache siasa za wazawa, tujikite kwenye tatizo la msingi

Mon, 26 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mpira unahitaji uwekezaji mkubwa, serikali ndio MDAU namba Moja katika Hilo. Wizara kuanza ku regulate idadi ya wachezaji huko ni kukwepa Majukumu ya Serikali ya msingi. Serikali imejenga academy ngapi??? Hata kama haijajenga imekaribisha wawekezaji wangapi wakubwa katika eneo Hilo ?

Wachezaji wazawa wanazalishwa wapi?

Yani atleast serikali ingekuwa imefanya uwekezaji mkubwa kidogo wangepata nguvu ya kutaka vijana wapewe nafasi, hizo nchi za waarabu zinatumia wazawa wengi lakini wametoka kwenye academy ambazo nyingine ni uwekezaji mkubwa wa serikali zao

Nchi Haina academy ya maana alafu unataka uishi kijima , tuna vijana wangapi wa level ya Mzize ? Au tunawaza tu kwa kuwa mtu ana miguu miwili basi anaweza kucheza mpira.

Morocco, Misri wanatumia wazawa wengi lakini Kuna miundombinu tayari ya kuzalisha vipaji vingi

Serikali licha ya kujenga tu, je imeweka mazingira rahisi kwa wawekezaji kuja kuwekeza katika michezo ?

Bajeti ya Wizara ni billion 30, bajeti ya Yanga ni Billion 20 , hakuna tofauti ya Serikali na klabu ya mpira hapo hapo unataka kuwapangia watu namna ya kuendesha Biashara yao

Kama serikali imeweka billion 30 maana yake mpira hauna faida kwa nchi au michezo sio kipaumbele

Inasikitisha watu wakubwa wenye ushawishi wanatoa maoni kwa hisia sio facts

Matokeo yake tunaleta Siasa kwenye michezo Yale Yale ya kufuta michezo mashuleni yanataka kujirudia tena Yani tuanze Leo kujadili idadi ya wazawa na wageni Ili Hali hatuna academy za kuzalisha wazawa wengi

Hao wazawa wanao pata nafasi kwenye hizo Yanga , Simba na Azam wanatosha kabisa kuunda National team kama focus yetu ni National team pekee , ila kama Focus yetu ni kukuza kiwango Cha wazawa basi tuanzie kwenye msingi ambao ni academy za kisasa

Serikali itoe ruzuku , watu wajenge academy, Timu za majeshi zenyewe hazina academy na hizo zipo chini ya Serikali

Kwanini tusianze na Timu za majeshi zote na Timu za Harimashauri zote ziwe za mfano , serikali iwekeze kwenye hizo Timu ziwe na shule za academy zizalishe wachezaji wengi

Baada ya hapo serikali itoe fursa kwa wawekezaji wakubwa ambao wanaweza kujenga academy kubwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live