Kiungo wa Ihefu, Papy Kabamba Tshishimbi huenda asirejee tena uwanjani katika michezo yote iliyosalia msimu huu baada ya kutakiwa kupumzika kutokana na kufanyiwa upasuaji mkubwa wa goti.
Kocha msaidizi wa Ihefu, Zubery Katwila alisema: “Kwa yeye kurudi msimu huu ni ngumu ndio maana tukaona ni vyema tumpe muda mwingi wa kupumzika ili arudi akiwa imara zaidi, hivyo tunararajia kuanzia sasa ataanza mazoezi mepesi mepesi tu.”
Kwa upande wa Katibu Mkuu wa Klabu hiyo, Zagalo Chalamila alisema baada ya Tshishimbi kufanyiwa upasuaji jijini Dar es Salaam aliomba kwenda kwao, hivyo kuanzia wiki hii atarudi nchini.