Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tshibamba atajwa kutua Simba

Screenshot 20190821 100502 Compressed Dago Tshibamba Samu

Mon, 28 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Imeelezwa kuwa Simba ipo katika mazungumzo ya mwisho na kiungo Mkongomani, Dago Samu Tshibamba anayekipiga klabu ya De Agosto ya nchini Angola.

Hiyo ni katika kuhakikisha wanakiboresha kikosi chao katika usajili huu wa dirisha dogo litakalofunguliwa Desemba, mwaka huu.

Simba wamepanga kuziboresha baadhi ya nafasi muhimu ambazo Kaimu Kocha Mkuu wa timu hiyo, Juma Mgunda ambazo amezipendekeza.

Kwa mujibu wa taaraifa ambazo imezipata Championi Jumatatu, nafasi ambazo zilizopendekezwa ni kiungo wa kati, kiungo wa pembeni na straika mmoja hatari.

Mtoa taarifa huyo alisema kuwa nafasi ya kiungo wa kati tayari wamempata Tshibamba ambaye wapo naye katika hatua za mwisho kukamilisha usajili wake.

Alisema kuwa uongozi hivi sasa wanakamilisha mazungumzo kati yake na meneja wa kiungo ikiwemo dau la usajili ambalo limefichwa hivi sasa.

“Tshibamba huenda akawa mchezaji wa kwanza kusajiliwa na Simba katika usajili wa dirisha dogo. Kwani ndiye mchezaji aliyependekezwa katika usajili wake na benchi la ufundi na uongozi, kwani waliwahi kumuona tulipokutana na De Agosto katika Ligi ya Mabingwa Afrika.

“Hivyo muda wowote usajili wake utakamilishwa kwa ajili ya kuiboresha safu ya kiungo,” kilisema chanzo hicho.

Mtendaji wa Simba, Barbara Gonzalez jana Jumapili alizungumzia usajili wa dirisha dogo na kusema kuwa: “Maamuzi makubwa yanakuja katika usajili wa dirisha dogo, wapo baadhi ya wachezaji tutakaowasajili na kuwaacha, Wanasimba muwe wavumilivu.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live