Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tshabalala ampiga bao Aziz Ki

Tshabalala: Tusikate Tamaa, Tutarudi Kwenye Ubora Wetu Tshabalala ampiga bao Aziz Ki

Tue, 26 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Licha ya kiungo wa Yanga, Stephane Aziz Ki kuwa kinara wa upachikaji wa mabao kufikia sasa msimu huu akitupia kambani mpira mara 10, unaambiwa beki kisiki wa Simba, Mohammed Hussein ‘Tshabalala amempiga bao kiungo huyo.

Iko hivi. Wakati Ligi Kuu Bara ikiwa imesimama kupisha ratiba ya michuano ya fainali za Mataifa ya Afrika 2023 beki wa Simba, Tshabalala ameonekana kucheza dakika nyingi zaidi kwa upande wa timu za Simba na Yanga akitumika kwa dakika 90 kwenye mechi kumi walizocheza.

Beki huyo kisiki ambaye ni panga pangua kikosini ametumika kwa dakika 90 kwenye mechi 10 zote walizocheza, pia mbali na Tshabalala staa mwingine wa Simba aliyecheza dakika nyingi akimfunika Aziz Ki ni Che Malone Fondoh (dakika 891), Shomari Kapombe (885), Fabrice Ngoma (881) huku kinara wa mabao Aziz Ki akicheza dakika 875.

Wakati ukuta wa Simba ukifunika kwa kucheza dakika nyingi kwa upande wa Yanga eneo la kiungo ndio limetumika zaidi baada ya Aziz Ki kuongoza kwa dakika nyingi akifuatiwa na kipa Djigui Diara ambaye amecheza dakika 810 huku beki Ibrahim Abdallah Hamad ‘Bacca’ akitumika kwa dakika 802.

Kiungo Maxi Nzengeli amecheza dakika 758 akishika nafasi ya nne, anafuatiwa na Dikson Job (720), Pacome Zouzoua ambaye amecheza dakika 714, Mudathir Yahya (673), Kouassi Yao (665), Khalid Aucho (629), Bakari Mwamnyeto (532), Joyce Lomalisa (495), Kennedy Musonda (492) Nikson Kibabage (439), Clement Mzize (388).

Yanga kwenye kikosi chao cha wachezaji 27 hakuna mchezaji ambaye amekosa nafasi ya kucheza huku waliocheza dakika chache wakiwa ni Chrispin Ngushi akicheza dakika 11, Jonas Mkude 14, Denis Nkane 40, Gift Fred 21, Faridi Mussa 65, Metacha Mnata 90, Abutwalib Mshery 90, Hafiz Konkoni 189, Mahlatsi Makudubela 166, Kibwana Shomari 240, Salum Abubakar 287 na  Zawadi Mauya 284.

Kwa upande wa Simba kuna wachezaji wao wanne ambao hawajaonja dakika hata moja kwenye Ligi Kuu Bara ambao ni Aubin Kramo ambaye ni majeruhi, Ahmed Feruz, Hussein Abel na David Kameta.

Waliocheza dakika chache zaidi ni Hussein Kazi dakika 5, Abdallah Hamis (chini ya 45), Jimson Mwanuke (chini ya 45), Shabani Chilunda 46, Israel Mwenda 30, Aishi Manula (90), John Bocco (199), Willy Onana (241), Moses Phiri, Luis Miquissone wote wamecheza dakika 287, Ayoub Lakred (360), Jean Baleke, Kibu Denis wamecheza dakika sawa (448), Sadio Kanoute (451), Keneddy Juma (430), Henock Inonga (474), Mzamiru Yassin (570), na Said Ntibazonkiza 753.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live