Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tshabalala alainishiwa maisha Simba Sc

Bocco Tshabalala Tshabalala alainishiwa maisha Simba

Wed, 26 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nahodha msaidizi wa Simba, Mohamed Hussien 'Tshabalala' amerahisishiwa kazi ya kupata namba kikosini baada ya timu hiyo kuachana na mpango wa kusajili beki mwingine wa kushoto.

Tshabalala aliyesaini mkataba mpya utakaomuweka Simba hadi 2025, awali alikuwa akiwania namba na Gadiel Michael aliyeachwa na kutimkia Singida Big Stars, na baada ya hapo Simba ilipanga kusajili beki mwingine atakayempa changamoto, lakini sasa mpango huo umekufa kutokana na mapendekezo ya kocha.

Mmoja wa viongozi wa Simba (jina tunalo) aliliambia gazeti hili kuwa kocha wa timu hiyo, Roberto Oliveira amewaambia wasihangaike kusajili beki mwingine wa kushoto, kwani kikosini ana watu zaidi ya wawili wanaoweza kucheza nafasi hiyo.

"Tulikuwa na mpango wa kusajili mchezaji katika nafasi hiyo, lakini hadi sasa hatujafanya hivyo kutokana na kocha kututuliza," alisema kiongozi huyo.

Alipoulizwa kuhusu nafasi hiyo, Robertinho alithibitisha kuukata uongozi wa Simba akisema kuna wachezaji wanaoweza kuimudu nafasi hiyo hata Tshabalala asipokuwepo.

"Ni eneo ambali kikosini tuna watu wanaweza kucheza, mabeki karibu wote wa kati wanaweza kucheza pembeni, pia kutokana na mifumo, hivyo hakuna shida juu ya hilo.

"Kama uliona mechi mbili za mwisho kwenye ligi alicheza Israh (Mwenda), kwenye nafasi ile na alifanya vizuri, na hivyo ndiyo nataka timu yangu iwe," alisema Robertinho.

Kwa maana hiyo ni rasmi sasa Mwenda aliyekuwa akishindania namba nafasi ya beki wa kulia na Shomari Kapombe sasa atahamia kushoto na kumuacha Kapombe akishindania namba na Davaid Kameta 'Duchu' aliyerejea

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: