Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tshabalala afunguka kambi ya Afrika Kusini

69190 Pic+tshabalala

Wed, 31 Jul 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Beki wa kushoto wa Simba, Mohammed Hussein 'Tshabalala' baada ya kufanya mazoezi ya nguvu Afrika Kusini ametoa maneno mazito ambayo wapinzani wakiyasikia ni hatari sana.

Tshabalala pia ni nahodha msaidizi wa Simba na leo Jumatano jioni, anatarajia kutua nchini pamoja na kikosi chake cha Msimbazi akitokea nchini humo.

Mchezaji huyo alisema wapinzani wao watakapouliza mambo yao yanakwendaje wajibu zaidi ya jana bila kuwataja ni akina nani anaowalenga.

Wapinzani wakubwa wa Simba kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara ni Yanga licha ya kuwa mashindano hayo yanashirikisha klabu 20.

"Mkiulizwa tunaendeleaje waambieni vizuri zaidi ya jana," alisema Tshabalala ambaye msimu huu atapambana na Gadiel Michael kuwania namba katika nafasi hiyo.

Simba iliweka kambi nchini humo tangu Julai 15 kwa maandalizi ya msimu mpya wa Ligi Kuu na Ligi ya Mabingwa Afrika.

Pia Soma

Katika mashindano ya Afrika, Simba itacheza mechi ya raundi ya kwanza dhidi ya UD Song ya Msumbiji.

Chanzo: mwananchi.co.tz