Nahodha Simba SC, Mohamed Hussein ‘Tshabalala' amesema kuwa kikosi chao kinajiandaa kikamilifu kwa ajili ya mchezo wa dabi dhidi ya watani zao, Yanga SC, Aprili 20 katika Dimba la Mkapa.
Tshabalala amesema hayo kuelekea mchezo huo muhimu huku Simba wakiwa wametoka kucheza mechi nne mfululizo bila kupata ushindi huku pia wakiwa na kumbukumbu ya kupoteza kwa bao 5-1 katika mchezo wa duru ya kwanza msimu huu dhidi ya Yanga.
“Lazima tukiri mchezo wetu ujao ni mgumu, lakini tutafanya kila jitihada kuhakikisha timu yetu inashinda. Tupo hapa Zanzibar kwa ajili ya kujiandaa kikamilifu ili kufikia malengo tuliojiwekea.
“Tunajua hatukufanya vizuri katika mechi zetu za nyuma hiyo haituvunji nguvu kwani tutaingia uwanjani kwa kufuata maelekezo aliyotupa mwalimu na kutimiza malengo tuliyojiwekea kwa timu na kujizolea pointi tatu muhimu," amesema Tshabalala.