Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tshabalala, Ninja gumzo mchangani

Zimbwe Mohamed Tshabalala Mtwara Mohamed Hussein "Tshabalala"

Sun, 25 Jun 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Ligi Kuu Bara imeisha, lakini mastaa wa timu mbalimbali wameendelea kujifua mchangani ili kujiweka fiti licha ya kuwa na mapumziko wakisubiri msimu mpya uanze na uwepo kwa wao umekuwa gumzo kwa mashabiki walioshindwa kwenda kuwaona kwenye mechi zao za Ligi Kuu.

Mwanaspoti lilitimba kwenye Uwanja wa Mpakani, uliopo Mabibo na kukuta nyomi la mashabiki wakiburudika kwam kuwaangalia mastaa wa hizo akiwamo Ayubu Lyanga (Azam FC), Shiza Kichuya (Namungo), nahodha msaidizi wa Simba, Mohamed Hussein 'Tshabalala', Athuman Miraj 'Sheva' (JKT Tanzania), Abdallah Shaibu 'Ninja' (Yanga), Juma Mahadhi na Juma Makapu(Ihefu).

Katika mazoezi hayo baadhi ya mastaa hao, mashabiki walisikika wakitaka Ibrahim Ajibu na msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini aliyewahi kusajiliwa Coastal Union, Ali Kiba nao waingie kwani ni kati ya mastaa wanaofanya mazoezi kwenye uwanja huo.

Mashabiki hao walisikika wakisema; "Tunapata wakati mzuri wa kuwatazama mastaa ambao wakati mwingine ni vigumu kuwaona live, wanapambana na kujituma kwa bidii kama wanavyofanya majukumu yao ya Ligi Kuu."

Lakini staa aliyeonekana kutajwa zaidi midomoni mwa mashabiki hao ni Kichuya kutokana na kasi ya kuzisakama nyavu ingawa ni kama alikuwa na bato kali na Ninja aliyekuwa anamuwekea vikwazo vya kufunga.

Kutokana na bato hiyo, walijikuta wakishangiliwa na mashabiki ambao walipenda ushindani wao, pia wengi walikuwa na hamu ya kumuona Ajibu alicheza ingawa Mwanaspoti liliondoka uwanjani hapo kabla ya kuingia staa huyo (Ajibu).

Chanzo: Mwanaspoti