Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tshabalala, Metacha watemwa Taifa Stars

98bce638ef2f3acee914161cf2e3004d.png Tshabalala, Metacha watemwa Taifa Stars

Tue, 5 Jan 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

KOCHA Mkuu wa timu ya soka ya taifa, Taifa Stars Ettiene Ndayiragije amewatema wachezaji Jonas Mkude, Mohamed Hussein ‘Tshabalala’ wa Simba na Metacha Mnata wa Yanga kwenye kikosi kitakachoriki fainali za michuano ya mabingwa wa Afrika (Chan) inayoshirikisha wachezaji wanaocheza ligi za ndani.

Michuano hiyo imepangwa kufanyika Cameroon Januari 16- Februari 7 mwakani. Kwa mujibu wa taarifa kutoka Shirikisho la soka Tanzania, TFF kwa waandishi wa habari jana, kikosi hicho kitaingia kambini Januari mosi, kujiandaa na michuano hiyo ambapo watacheza mechi mbili za kirafiki za kimataifa dhidi ya DR Congo kabla ya kuanza safari kwenda Cameroon.

Pengine ni hali ya kushangaza kuwaacha Mkude, Tshabalala na Mnata ambao kwa sasa wanafanya vizuri kwenye timu zao katika Ligi Kuu Bara. Kwa mara ya kwanza kwenye kikosi hicho yamefanyika maboresho makubwa kwa kuwajumuisha wachezaji wengi vijana huku wakongwe wakiachwa.

Wachezaji wengine walioitwa na Ndayiragije ni Aishi Manula, Shomari Kapombe, Erasto Nyoni , Said Ndemla,John Bocco wa Simba, Yassin Mustapha, Bakari Mwamnyeto,Feisal Salum, Ditram Nchimbi, Deus Kaseke, Farid Mussa, wa Yanga.

Agrey Morris,Ayoub Lyanga , Khelflinnie Salum, Pascal Gaudence wa Azam FC, Juma Kaseja na Israel Mwenda wa KMC na Dan Mgore kutoka Biashara United. Wengine ni Abdultwalib Mshery, Baraka Majogoro, Dickson Job, wa Mtibwa Sugar, Edward Manyama,Carlos Protasi,Lucas Kikoti, wa Namungo FC na Yussufu Mhilu wa Kagera Sugar.

Samweli Jackson wa Ihefu FC na Abdulrazack Hamza wa Mbeya City ,Adam Adam wa JKT Tanzania ,Rajabu Athuman kutoka Gwambina FC na Omari Abbasi (U17).

Chanzo: habarileo.co.tz