Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Try Again kutangulia Guinea

Try Again, Salim Abdallah Try Again kutangulia Guinea

Mon, 6 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi Simba, Salim Abdallah ‘Try Again’ yupo Morocco kwa ajili ya mambo mawili makubwa ya kuinufaisha klabu hiyo.

Jambo la kwanza Try Again ni miongoni mwa wawakilishi wachache kutokea Afrika ambao wataudhuria mkutano wa Shirikisho la soka duniani (FIFA), kuhusu mambo mbalimbali ya soka la dunia.

Baada ya hapo Try Again atakuwa na kikao cha Shirikisho la soka Afrika (CAF), kuhusu mambo mbalimbali ya soka la Afrika ikiwemo mashindano ya (Super League), ambayo yataanza hivi karibuni.

Jambo lingine litakalojadiliwa ni masuala ya bajeti nzima na kila timu itakayoshiriki inatakiwa kupata kiasi gani ili kujikimu kabla na baada ya mashindano.

Haraka baada ya kumaliza mambo hayo mawili Try Again atachukua ndege na kutua Guinea kwa ajili ya kuunganisha nguvu na Mratibu wa timu, Abasi Ally kwa ajili ya kuweka mazingira sawa.

Kuna mambo ya msingi Try Again atayaweka sawa Guinea kwa ajili ya kuhakikisha kikosi baada ya kufika siku mbili kabla ya mchezo kukutana na mazingira yote mazuri yapo tayari.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live