Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Try Again: Simba vs Al Ahly ni mechi ya Watanzania wote

Simba Jeziiiiiii Try Again: Simba vs Al Ahly ni mechi ya Watanzania wote

Wed, 18 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi wa Klabu ya Simba, Salim Abdallah 'Try Again' amesema kuwa mchezo wao wa robo fainali ya African Football League (AFL) dhidi ya AL Ahly sio mchezo wa Simba pekee bali Taifa zima la Tanzania.

Try Again amesema hayo kuelekea mchezo huo utakaopigwa keshokutwa Ijumaa, Oktoba 20, 2023 katika Dimba la Mkapa jijini Dar es Salaam.

"Tunafahamu Al Ahly ni timu kubwa, ni mabingwa wa Afrika, tunawaheshimu. Lakini Simba sio wadogo, ni miongoni mwa klabu nane [8] bora Afrika, kwa hiyo tunao uwezo wa kupambanao na kupata matokeo.

"Nawaomba watanzania hii ni mechi ya watanzania wote sio mechi ya Simba, kwa hiyo nawaomba watanzania waje kwa wingi uwanjani kuiunga mkono timu yao ya Simba ambayo itakuwa inaiwakilisha Tanzania.

"Kwa hiyo wanunue tiketi waje uwanjani, nilikuwa naangalia mauzo ya tiketi tayari tumevuka 60%. Watu waje kuangalia burudani za ufunguzi wa mashindano haya ambayo imeandaliwa kwa kiwango cha zaidi ya sherehe za AFCON," amesema Salim Abdallah.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live