Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Try Again - Ndoto yetu kufika fainali

7X9A8896 Kikosi cha Simba

Tue, 15 Mar 2022 Chanzo: eatv.tv

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Simba Salim Abdallah,’Try Again’amesema kuwa malengo ya timu hiyo kimataifa ni kufanya vizuri na hata kufika fainali kwenye michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika msimu huu.

Simba ambayo inaongoza kundi D ikiwa na alama 7 baada ya kucheza mechi 4 inafuatiwa na Asec Mimosas iliyo nafasi ya pili na pointi 6 kibindoni.

”Malengo yetu ni kuweza kufanya vizuri kwenye mechi zetu ambazo tunacheza kimataifa na lengo ni kuona tunapata matokeo mazuri na kufika mbali maana ushindani ni mkubwa hilo tunalijua lakini sisi tuna uzoefu wa kutosha naamini tufanya vizuri msimu huu''amesema Try Again.

Mchezo ujao wa Simba kimataifa ni dhidi ya ASEC unatarajiwa kuchezwa Jumapili ya Machi 20 itakuwa ugenini.

 

Chanzo: eatv.tv