Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Try Again, Injinia Hersi waitwa CAF

Hersiii WA0017 Try Again, Injinia Hersi waitwa CAF

Wed, 29 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baadhi ya wenyeviti na watendaji wakuu wa klabu mbalimbali watakuwepo Cairo, Misri kwa ajili ya kuhudhuria uanzishwaji wa Chama cha Klabu za Soka Afrika (ACA), Novemba 30 mwaka huu.

Uzinduzi rasmi wa Chama hicho utaongozwa na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) na utafanyika katika Hoteli ya Marriot Mena House, Cairo kuanzia saa 6 mchana.

Uzinduzi huo utafuatiwa na mkutano wa waandishi wa habari ambao utaongozwa na Motsepe na wanachama wa ACA.

Chama hicho cha ACA kimeanzishwa ili kutimiza malengo matano la kwanza likiwa ni kulinda na kupandisha maslahi ya klabu za soka Afrika.

Lengo la pili ni kuhakikisha klabu za soka Afrika zinakuwa na hali nzuri kiuchumi ambayo itaziwezesha kushindana na kupata faida.

Kuhakikisha waamuzi, makamishna na wasimamizi wa teknolojia ya usaidizi wa video kwa marefa (VAR) wanaheshimiwa, wanakuwa huru, wanaaminika na kuwa na na daraja la dunia ni lengo la tatu la kuanzishwa kwa chama hicho.

Lengo la nne ni kujenga ushirika na wadhamini, sekta binafsi na serikali kujenga viwanja ambavyo vinaendana na hadhi ya CAF na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (FIFA) na miundombinu mingine ya mpira wa miguu na vigaa kwa kila nchi mwanachama CAF.

Kukuza vipaji vya vijana wa Kiafrika, akademi kwa wavulana na wasichana na kuimarisha ubora wa soka la klabu Afrika kuwa katika ngazi ya kidunia ni lengo la tano la uanzishwaji wa ACA.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live