Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Trippier awakataa Casemiro, Partey mbele ya Decline Rice

Casemirox Rice N Partey.jpeg Viungo wanaotamba EPL kwa sasa

Thu, 9 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Beki wa kulia wa kimataifa wa Uingereza anayekipa kwenye klabu ya Newcastle Kieran Trippier amesema kua kiungo wa klabu ya West Ham Declan Rice ni bora kuliko kiungo wa Manchester United Carlos Casemiro.

Kiungo Declan Rice amekua kwenye kiwango bora kwa miaka takribani mitatu sasa ndani ya klabu ya West Ham kitu kilichofanya Trippier aamini kua kiungo huyo ni bora zaidi ya viungo kama Carlos Casemiro pamoja kiungo wa Arsenal Thomas Partey.

Declan Rice ambaye siku kadhaa nyuma kocha wake David Moyes alizungumza kua huenda ukaenda kua usajili ambao utavunja rekodi ndani ya Uingereza kama ataondoka ndani ya klabu ya West Ham, na kauli hiyo inatokana na kiwango ambacho anaonesha kiungo huyo.

Beki Trippier ambaye alifanya mazungumzo na na beki wa zamani wa klabu ya Manchester United Rio Ferdinand alisema kua hataki kuwakosea heshima Casemiro na Partey, Lakini anaamini kwa sasa Declan Rice ni bora zaidi kutokana na namna anavyocheza na anavyotembea na mpira ni maajabu.

Kiungo Declan Rice amekua akihusishwa kuondoka ndani ya klabu ya West Ham na mkataba wake upo mwishoni na vilabu kama Manchester United, Arsenal, na Newcastle vinatajwa sana kuwania saini ya kiungo huyo wa kimataifa wa Uingereza.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live