Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Trippier astaafu soka la Kimataifa

Kevin Trippier Trippier astaafu soka la Kimataifa

Thu, 29 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Beki wa Newcastle United Kieran Trippier ametangaza kustaafu kucheza mpira wa miguu timu ya taifa England.

Amechukua uamuzi huo baada ya kusaidia timu ya taifa kufika fainali ya Michuano ya Kombe la Ulaya-Euro 2024 iliyopigwa Agosti 14, Ujerumani huku Hispania ikitwaa ubingwa.

Trippier mwenye umri wa miaka 33 amecheza mechi 54 timu ya taifa England akifunga bao moja pekee wakati wa mchezo wa nusu fainali Kombe la Dunia 2018 jijini Moscow, Urusi dhidi ya Croatia ambapo nchi yake ilipoteza.

"Imekuwa moja ya heshima kubwa zaidi maishani mwangu kuiwakilisha nchi yangu kwenye mashindano makubwa manne. Ningependa kutoa shukrani kubwa kwa Gareth na benchi lote la ufundi lililokuwa na kikosi cha England kwa kuniamini kwa miaka yote."

Beki huyo wa kulia wa Newcastle, ambaye alianza kucheza timu ya taifa mwaka 2017 chini ya kocha wa zamani Gareth Southgate, alivaa kitambaa cha unahodha mara 3.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live