Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tresor Mputu kutundika daruga Mazembe

Tresor Mputu Tresor Mputu kutundika daruga Mazembe

Mon, 13 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Staa wa TP Mazembe, Tresor Mputu ametokwa na machozi wakati akiwaaga rasmi mashabiki wa Klabu hiyo kwenye mchezo wao dhidi ya Real Bamako jana Jumapili February 12, 2023.

Tresor Mputu ambaye amejiunga na TP Mazembe mwaka 2002 ametoa heshima zake za mwisho kwa mashabiki wa timu hiyo baada ya kutangaza kustaafu mchezo wa soka Februari 9, 2023 akiwa na umri wa miaka 37.

Tukio hilo limefanyika kabla ya mechi ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika baina ya TP Mazembe na Real Bamako ambapo wenyeji Mazembe waliibuka na ushindi wa goli 3-1.

Legend huyo, Tresor Mputu anapata mafanikio makubwa kwenye soka la Bara la Afrika ikiwemo Mfungaji Bora wa CAF Champions League 2009 kwa kufunga magoli tisa, Ubingwa wa CHAN, CAF Champions League, CAF Confederation Cup, World top scorers of the year kwa mujibu wa IFFHS.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live