Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Trent, Foden wazia gumzo England

TAA.jpeg Trent Alexander Arnold

Sun, 27 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wachezaji wa timu ya taifa ya Uingereza Phil Foden na Trent Alexender Arnnold wamezua gumzo kwa mashabiki wa timu ya taifa ya England baada ya kuwekwa benchi kwa wachezaji hao.

Mashabiki wengi wa timu hiyo wakiongozwa na wachezaji wa zamani wa timu hiyo wameonesha kutokufurahishwa na maamuzi ya mwalimu Gareth Southgate baada ya kuwaweka wachezaji hao nje na timu hiyo kushindwa kupata matokeo katika mchezo wa jana dhidi ya Marekani.

England juzi walipata sare na timu ya taifa ya Marekani huku wwakionekana kuzidiwa katika mchezo huo. Jambo hili ndo limefanya watu kuhoji kwanini Foden na Trent wawekwe benchi katika mchezo huo.

Magwiji kama Michael Owen ambaye amewahi kuitumikia timu hiyo ameonesha kusikitishwa na kitendo cha Southgate kuwaweka benchi wachezaji hao na kusema hawjapata matokeo mazuri lakini wachezaji wao wenye vipaji vikubwa wamewekwa nje.

Phil Foden na Trent Arnold wamekua wachezaji muhimu zaidi kwenye vilabu vyao lakini inakua tofauti wakienda kwenye timu ya taifa ya Uingereza ambapo wamekua wakipata nafasi finyu ndani ya timu hiyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live