Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tottenham yakamilisha usajili wa Eberechi Eze

Eberechi Eze Eberechi Eze.

Wed, 26 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Tetesi za usajili zinasema Tottenham ina nia kumsajili fowadi wa Crystal Palace Eberechi Eze, 25, na huenda ikaangalia uwezekano wa kuhuisha kipengele cha kuachiwa cha mkataba wake. (Talksport).

Brighton & Hove Albion inakusudia kumsajili kiungo wa Leicester City, Kiernan Dewsbury-Hall, 25.(Telegraph - subscription required) Arsenal imeulizia kuhusu kumsajili fowadi mbelgiji wa PSV Eindhoven Johan Bakayoko, 21. (DHNet - in French).

Aston Villa inafikiria uhamisho wa winga wa Sporting Lisbon, Pedro Goncalves,25. (A Bola - in Portuguese).

Ipswich Town ipo katika mazumgumzo ya hali ya juu na beki Ben Johnson, 24, kuhusu uhamisho huru wakati mkataba wake katika klabu ya West Ham utakapomalizika wiki ijayo. (East Anglian Daily Times).

Manchester United imefanya mazumngumzo na Juventus kuhusu kumsajili kiungo Adrien Rabiot,29, lakini inakabiliwa na ushindani kutoka Arsenal na Aston Villa. (Teamtalk).

Chanzo: www.tanzaniaweb.live