Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tottenham Wamgeukia Marco Asensio

Asensio.jpeg Winga wa Real Madrid, Marco Asensio

Sun, 10 Apr 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Tottenham Hotspur ni miongoni mwa vilabu ambavyo vimefanya mawasilioni na wakala wa Marco Asensio kuhusu uwezekano wa kupata saini yake kwenye majira ya kiangazi ambapo klabu ya Real Madrid wanatarajia kumuweka sokoni mwishoni mwa msimu.

Marco Asensio mpaka sasa ameichezea klabu hiyo michezo 26 huku akiwa ameanza kwenye michezo 15 msimu huu. Japokuwa kuna sintofahamu kati yake na klabu ya Madrid na kupelekea kuwekwa sokoni mwisho wa msimu.

Mkataba wa Asensio na Madrid unamalizika mwaka 2023, mpaka sasa amekataa mkataba ambao klabu hiyo imemuandalia, ndio maana wanataka kumuweka sokoni mwishoni mwa msimu ili kuweza kupata pesa na kuzui kutompoteza bure baada ya msimu huu kuisha na wako tayari kusikiliza ofa inayoanzia Pauni milioni 30.

Kulingana na taarifa zilizopo ni klabu mbili tu mpaka sasa kutoka Uingereza ambazo zimefanya mawasiliano na wakala wa Asensio kuhusu kupata huduma yake ambazo ni Tottenham na Arsenal.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live