Ni majuto tu upande wa Tory Lanez, taarifa zinaeleza kwamba mkali huyo wa muziki toka nchini Canada anapitia nyakati ngumu sana kwenye maisha yake na anajutia kwanini hakukiri makosa yake Mahakamani mwezi Disemba.
Ni majuto tu upande wa Tory Lanez, taarifa zinaeleza kwamba mkali huyo wa muziki toka nchini Canada anapitia nyakati ngumu sana kwenye maisha yake na anajutia kwanini hakukiri makosa yake Mahakamani mwezi Disemba. Tovuti ya Rolling Stone imeandika taarifa hiyo wakati Tory Lanez akiwa rumande kwa sasa akisubiri hukumu yake ambayo itasomwa February 28 mwaka huu ambapo huwenda akahukumiwa kifungo cha miaka 22 na miezi 8 Jela.