Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Top Six EPL na matumizi ya noti

Higheste Paid Top Six EPL na matumizi ya noti

Sun, 5 Mar 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Kazi ya pesa ni matumizi hasa ukiwa nazo. Na hilo ndilo linalofanywa na Manchester United baada ya kufunika klabu nyingine zote kwenye Ligi Kuu England kwenye upande wa kulipa mishahara mikubwa mastaa wake.

Ni hivi, Man United ndiyo timu yenye bili kubwa zaidi ya mishahara kuliko timu nyingine yoyote kwenye Ligi Kuu England, licha ya kwamba kwa sasa wanapambana kuwamo kwenye moja ya timu zinazoshindania ubingwa kwenye lig hiyo kama ilivyo kwa mahasimu wao Manchester City.

Klabu za Ligi Kuu England zilifichua vitabu vyao vya hesabu vya msimu wa 2021/22 na namba zilionyesha kwamba Man United ndio waliokuwa na bili kubwa ya mishahara ya Pauni 384 milioni.

Kwenye hesabu hizo, supastaa Cristiano Ronaldo alikuwa bado yupo kwenye kikosi cha Man United, ambapo mshahara wake alikuwa akilipwa Pauni 480,000 kwa wiki. Hiyo ilikuwa msimu uliopita tu hapo.

Lakini, Ronaldo aliondoka na sasa yupo Al-Nassr alikwenda kujiunga Desemba mwaka jana, huku jambo hilo likimfanya kipa David De Gea, awe mchezaji anayelipwa mshahara mkubwa zaidi huko Old Trafford, Pauni 375,000 kwa wiki.

Man United inafuatiwa na Liverpool, ambao wao bili yao ya mishahara iliongezeka kwa asililia 75 kwa kuanzia mwaka 2017. Liverpool yenyewe ilirekodi faida ya Pauni 7.5 milioni tu kabla ya kodi kwa msimu uliopita na hivyo kushika namba mbili wakiwapiku Man City kwa kuwa na bili kubwa ya mishahara.

Mikataba mipya ya mastaa kama Andy Robertson, Fabinho, Jordan Henderson, Virgil van Dijk na Trent Alexander-Arnold ndiyo iliyopandisha bili hiyo, sambamba na dili jipya la supastaa Mohamed Salah, anayelipwa Pauni 350,000 kwa wiki.

Hilo limefanya Liverpool kuzidiwa Pauni 18 milioni tu kwenye bili yao ya mishahara dhidi ya Man United, ambapo kwa mwaka 2017, pengo la bili ya mishahara baina yao, lilikuwa Pauni 56 milioni.

Man City wao bili yao ya mishahara kwa mwaka ni Pauni 354 milioni, wakiwazidi Chelsea, ambao bado hawajaweka bayana vitabu vyao vya hesabu vya msimu uliopita.

Kwenye kikosi cha Man City, supastaa Kevin De Bruyne, ndiye anayelipwa mkwanja mrefu, akipokea Pauni 400,000 kwa wiki, huku huko Stamford Bridge kwenye maskani ya The Blues, Kai Havertz, akiwa bosi wao kwa kulipwa mshahara mkubwa, Pauni 310,00 kwa wiki.

Huko kwingineko, Tottenham Hotspur imewafunika mahasimu wao wa London Kaskazini, Arsenal kwa kulipa mishahara mikubwa mastaa wake. Spurs bili yao ya mishahara imepongezeka kwa asilimia 66 kutoka Pauni 127 milioni mwaka 2017 hadi Pauni 209 milioni.

Arsenal bili yao ya mishahara pia imeongezeka, lakini yao imetoka Pauni 195 milioni hadi Pauni 206 milioni.

Kwenye kikosi hicho cha Emirates, kiungo Thomas Partey ndiye aliyekuwa akilipwa mshahara mkubwa Arsenal, lakini ujio wa Gabriel Jesus umekuja kumnyang’anya ubosi baada ya Mbrazili huyo kupokea Pauni 265,000 kwa wiki baada ya kutua akitokea Man City mwaka jana.

BILI YA MISHAHARA YA KLABU ZA BIG SIX KWA MSIMU 2021/22

1. Man United – Pauni 384 milioni (imepanda asilimia 45)

2. Liverpool – Pauni 366 milioni (imepanda asilimia 75)

3. Man City – Pauni 354 milioni (imepanga asilimia 34)

4. Chelsea – Pauni 333 milioni (imepanda asilimia 51)

5. Tottenham – Pauni 209 milioni (imepanda asilimia 66)

6. Arsenal – Pauni 206 milioni (imepanda asilimia 5.6)

Chanzo: Mwanaspoti