Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

‘Top 4’ yamtoa mate Ouma, aiona coastal union CAFCL

Coastal Union Ligi Leo.jpeg ‘Top 4’ yamtoa mate Ouma, aiona coastal union CAFCL

Tue, 23 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Mkuu wa wagosi wa kaya Coastal Union, David Ouma ameweka wazi kuwa kuwa anazitaka nafasi tatu za juu wasipofanikiwa hilo basi wamalize msimu wa 2024/25 wakiwa nafasi ya nne.

Coastal Union wapo kambini kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Kombe la Shirikisho Afrika pamoja na mchezo wao wa Ngao ya Jamii dhidi ya Azam FC, Agosti 8, mwaka huu, Visiwani Zanzibar.

Ouma ameiambia Spotileo kuwa maandalizi yao kwa ajili ya msimu wa 2024/25 na hayaangalii mchezo mmoja dhidi ya Azam FC wa ngao ya jamii bali anahitaji kuona timu hiyo inafanya vizuri katika kila mashindano yote ya msimu ujao.

“Ngao ya Jamii ni mchezo wa mtoano tunahitaji kufanya vizuri sio mbele ya Azam FC bali kuangalia mashindano yote na ikiwezekana kupambana kutafuta nafasi tatu za juu ikishindikana basi bora tusalie nafasi ya nne, mwisho wa msimu,” amesema Kocha huyo.

Ameongeza kuondolewa mapema kwenye michuano ya Kagame kumemsaidia kuona mapungufu ya kikosi chake ili afanyie kazi kabla ya msimu mpya unaoanza Agosti 16, mwaka huu.

Ouma amesema ana kikosi chenye wachezaji wazuri na kutarajia kufanya vizuri kwenye mashindano yote yaliyopo mbele yao ikiwemo mchezo wa Ngao Jamii dhidi ya Azam FC.

“Hautakuwa mchezo rahisi kwa sababu kila mmoja anataka kucheza fainali, tumesajili wachezaji wazuri na matumaini yangu ni kupata matokeo mazuri kwenye mchezo huo na kufikia malengo yetu mwishoni mwa msimu,” amesema Kocha huyo

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: