Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Toni Kroos aweka rekodi Klabu Bingwa ya Dunia

Toni Kroos Club World Cup.jpeg Toni Kroos

Sun, 12 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiungo wa klabu ya Real Madrid Toni Kroos amefanikiwa kuweka rekodi ya kua mchezaji aliyetwaa taji la klabu bingwa ya dunia kuliko mchezaji yeyote baada ya kutwaa ubingwa huo siku ya jana.

Toni Kroos ambaye alianza kwenye kikosi kilichocheza dhidi ya Al-Hilal katika mchezo wa fainali wa klabu bingwa ya dunia na kufanikiwa kutwaa ubingwa huo. Kiungo huyo anaingia kwenye vitabu vya historia baada ya kua mchezaji wa kwanza alietwaa ubingwa wa klabu bingwa ya dunia kwa mara sita.

Kiungo huyo ambaye amefanikiwa kutwaa mataji hayo akiwa na vilabu viwili tofauti ambavyo ni klabu ya Bayern Munich pamoja na klabu ya Real Madrid kwa miaka tofauti taofauti akiwa anavitumikia vilabu hivo. Jana akifanikiwa kua kinara baada ya Real Madrid kuibamiza Al-Hilal kwa mabao matano kwa matatu kwenye mchezo wa fainali.

Toni Kroos ametwaa taji la klabu bingwa ya dunia mara moja akiwa na klabu ya Bayern Munich mwaka 2013 huku akitwaa mara tano na klabu ya Real Madrid miaka ya 2014,2016,2017,2018, na 2023 ni wazi usiku wa jana ulikua mzuri sana kwa kiungo huyo.

Toni Kroos ikumbukwe pia yupo kwenye orodha ya wachezaji waliotwaa ubingwa wa ulaya mara nyingi ambapo tayari akiwa ametwaa ubingwa huo mara tano mpaka sasa, Akitwaa taji hilo na Bayern Munich mwaka 2013 pamoja mataji manne akiw andani ya Real Madrid miaka ya 2016,2017,2018 na mwaka 2022.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live