Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Todibo kupishana na Varane Man Utd

Image 99 1140x640.png Todibo kupishana na Varane Man Utd

Thu, 9 Nov 2023 Chanzo: Dar24

Klabu ya Manchester United imepanga kumsajili beki wa kati wa Nice, Jean-Clair Todibo, ili akawe mbadala wa mchezaji mwenzake raia wa Ufaransa, Raphael Varane ambaye anadaiwa kuwa huenda akatimkia Saudi Arabia katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi.

Ili kuipata huduma ya Todibo mwenye umri wa miaka 23, taarifa zinadai Nice inahitaji walau Pauni 50 milioni kwa staa huyo ambaye mkataba wake unatarajiwa kumalizika mwaka 2027.

Varane mwenye umri wa miaka 30 amekuwa kwenye rada za vigogo mbalimbali Saudia tangu dirisha lililopita la majira ya kiangazi lakini Man United ilikataa kumuuza.

Hata hivyo, mpango wa Man United wa kutaka kuendelea kuwa naye kwa sasa unadaiwa kubadilika kwani beki huyo amekuwa akikumbwa na majeraha ya mara kwa mara katika kipindi cha hivi karibuni hali inayosababisha asipate muda mwingi wa kucheza.

Todibo tangu kuanza kwa msimu huu amecheza mechi 10 za michuano yote na kutoa asisti moja wakati Varane naye amecheza mechi 10 za michuano yote.

Chanzo: Dar24