Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tizi la Singida usipime

Singida Fountain Gate Tizi Tizi la Singida usipime

Sun, 27 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kikosi cha Singida Fountain Gate tayari kipo jijini Dar es Salaam kujiandaa na mechi ya marudiano ya raundi ya awali ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya JKU ya Zanzibar, na jana walijifua kwenye Uwanja wa Uhuru, huku wakionyesha wamepania kuimaliza JKU kesho Jumapili.

Makocha wa timu hiyo wakiongozwa na Hans Pluijm waliwapigia tizi la maana mastaa wa timu hiyo huku mzigo ukiwa kwa wale wanaocheza eneo la kiungo na ushambuliaji waliopewa kazi ya zaida.

Singida itavaana na JKU kesho kwenye Uwanja wa Azam Complex, baada ya wikiendi iliyopita kushinda mabao 4-1 uwanjani hapo ikishiriki michuano ya CAF kwa mara ya kwanza baada ya kupanda Ligi Kuu msimu uliopita kutoka Championship.

Viungo Morice Chukwu na Marouf Tchakei walipigishwa tizi la maana la kutengeneza na kupiga pasi za mwisho zilizotakiwa kufika eneo la ushambuliaji lililoongozwa na straika Mkongo Fancy Kazadi na Meddie Kagere.

Eneo hilo la kati lilioneka kuwa bora kwa aina ya udambwidambwi iliyokuwa kwani licha ya  kutengeneza nafasi, lakini pia walikuwa wakifunga wenyewe, japo shida ilikuwa kwa Mbrazil Bruno Gomez ambaye hakuwa sawa hasa kwenye kupiga mipira mirefu na kupiga mashuti.

Kazadi na Kagere walitumia karibu kila pasi alizopewa na viungo hao hasa kutoka kwa Chukwu na kufunga mabao jambo lililomfurahisha kocha Hans, ingawa Habib Kyombo alitengeneza mipira mitano na kutupia moja tu kimiani, tofauti na Kazadi alitengenezewa tano na kufunga  nne.

Wengine waliong’ara kwa kutumia nafasi walizotengenezewa ni Thomas Ulimwengu na Dickson Ambundo aliyekuwa tishio eneo la winga akiwa amepiga mipira ya krosi mitatu ya hatari.

Kocha wa timu hiyo, Pluijm aliliambia Mwanaspoti baada ya mazoezi hayo kuwa, lengo la timu ni kuwa bora eneo la ushambuliaji na kufunga ili kupata matokeo mazuri ya haraka na kutopoteza nafasi hovyo.

Pluijm alisema ametumia mawinga ili kuwaboreshea uwezo mzuri wa kupiga krosi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live