Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Wanawake 'Twiga Stars' Bakari Shime ametaja kikosi cha wachezaji 30 huku Yanga Princess ikitoa wachezaji tisa (9) na JKT Queens saba (7)
Kikosi hicho kitaingia kambini Aprili 2 mwaka huu kujiandaa na mchezo dhidi ya Kenya.
Katika kikosi hicho wachezaji walioitwa kutoka Yanga Princess ni Husna Mtunda, Zulfa Makau, Maimuna Kaimu,Janeth Christopher, Irine kisisa, Lucia Mrema, Emiliana Mdimu, Famukazi Ally na Amina Ally.
JKT Queens walioitwa ni kipa Najat Abas, Anastazia Katunzi, Happy Hezrone, Stumai Abdallah, Donisia Minja, Jackline Shija na Eto Mlenzi.
Wachezaji wengine walioitwa ni mabeki wa Fountain Gate Princess, Protasia Mbunda na Ester Mabanza.
Katika kikosi hicho Simba Queens imetoa wachezaji wanne ambao ni kipa,Gelwa Yona, Ester Mayala, Amina Ramadhan na Fatuma Issa.
Wachezaji wa kulipwa walioitwa ni Ezekia Kasongo kutoka timu ya Ausfaz ya Morroco, Julieth Singano Juarez (Mexico) Opa Clement Besiktas (Uturuki), Aisha Masaka BK Hacken (Sweden)Fatuma Mwisendi Nees Atromitou(Ugiriki), Zuwena Aziz Nahaj Sous (Morroco).
Katika kikosi hicho pia amejumuishwa Anatoria Audax kutokea The Tiger ya Jijini Arusha.