Makocha wamekuwa wakipewa mzigo wa lawama pale timu ambapo inashindwa kufanya vizuri. Si vibaya kwa kuwa kila kocha anapewa malengo ya kufanya.
Jambo la msingi kuzingatia kwenye suala la kuwapa mkono wa asante ni kuangalia nammna bora ya kukaa na benchi la ufundi kwa muda pamoja na malengo hayo yanavyoweza kufanikiwa.
Kitu kikubwa ni kuangalia kwenye suala la usajili nani ambaye anasimamia hilo? Yale ambayo yalipendekezwa kwenye ripoti yalifanyiwa kazi au ni porojo tu?
Ili benchi la ufundi lifanye kazi kwa umakini ni muhimu kuwa na watu wenye uwezo unaondena na kasi husika. Ipo wazi kuwa wapo makocha ambao wanapewa kila kitu lakini mbinu zinawakataa hao ni muhimu kukaa nao na kuangalia namna ya kuwa mkono wa asante.
Pia wakati wa kuvunja mikataba ni muhimu utaratibu ukazingatiwa kuokoa kesi wakati ujao. Masuala ya kuachana na makocha kwa mdomo hii ni hasara kubwa kwa timu husika.
Wachezaji nao wanatambua hali halisi ilivyo ni muhimu kujituma kutumia nafasi zinazopatikana ili kutimiza majukumu yao ndani ya uwanja.
Wakati mwingine anabebeshwa lawama kocha ilihali wachezaji nao wanafanya makosa ambayo hawakufundishwa.
Makosa yapo lakini lazima yafanyiwe kazi kwenye mechi za ushindani. Ligi ni ngumu kila timu inapambana kupata pointi tatu hivyo lazima kufanya yote kwa umakini ili kupata kilicho bora.