Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Timua timua ya makocha izingatie makubaliano ya pande zote

Pluijm X Robertinho Timua timua ya makocha izingatie makubaliano ya pande zote

Thu, 7 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ile kauli ya makocha wanaajiriwa ili wafukuzwe isiwe kigezo cha kila timu kumfukuza kocha pale wanapokosa wanachokitarajia kwenye mechi husika.

Ipo wazi kuwa kuna mengi ambayo yanamzunguka kocha kwenye mpango kazi wa kusaka matokeo. Inawezekana viongozi wanatambua makosa yalipo wanashindwa kuyatatua kwa wakati.

Muda mwingine ni aina ya wachezaji waliopo kushindwa kwenda na kasi iliyopo ama uwezo wao kuwa mdogo kulingana na aina ya mashindano ambayo wanashiriki.

Hakuna namna kwa timu ambayo ilifanya usajili kwa ujanjaujanja kinachotokea uwanjani sio mali ya kocha ni timu nzima kiujumla hapo wanapaswa kufanya tafakari kubwa kwa wakati ujao.

Ila kama kila kitu kilifanywa na benchi la ufundi likiwa linatambua kinachoendelea basi kinachotokea benchi la ufundi ni muhimu kuwajibika.

Katika kuwajibishwa kwa benchi la ufundi muhimu kuzingatia makubaliano ambayo yapo kwenye mkataba kuhusu malipo.

Kuna timu ambazo ziliingia migogoro baada ya kusitisha mikataba na makocha waliokuwa wanazinoa timu zao na mwisho wakafungiwa kujihusisha na usajili mpaka watakapokamilisha malipo.

Hili ni jambo la msigi kuangalia pia kwenye vipengele vya mikataba. Sio kwa makocha tu hata wachezaji ni muhimu utaratibu ukafuawa.

Kufuatwa kwa utaratibu kutapunguza kesi ambazo hazina faida kwa timu zaidi ya kuongeza gharama kwenye upande wa matumizi ya fedha na faini ambazo zitafanya mipango mingine isiendelee.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: