Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Timu zimegoma kupishana na Yanga sasa hivi - Ambangile

Yanga Mudathir Guede Timu zimegoma kupishana na Yanga sasa hivi

Thu, 9 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Aina ya pointi tatu ngumu ambazo huwa zinaenda kutafsiri hatua zako kuelekea kwenye ubingwa, hatua moja zaidi Yanga SC wamepiga.

Minziro alijua hakuna namna ambayo atapishana na Yanga na kupata matokeo chanya, na alijua nguvu ya Yanga ipo wapi zaidi (ni ndani zaidi kuliko pembeni ya uwanja) na ndio maana set up ya team yake ilikuwa mahususi kukabiliana na hiyo nguvu ya Yanga.

1: Block ya chini kabisa ya 4-4-2 ambayo inazuia ndani zaidi ili kuwalazimisha Yanga pembeni ya uwanja.

2: Kwenye penati box lao walihakikisha mabeki wote wanne wapo na mbele yao viungo ambao wapo tayari kuwania mipira ya pili.

3: Hatua inayofuata ilikuwa ni jinsi gani ya kutumia counter attacks, shida ilikuwa ni kwamba muundo wa ulinzi wa Yanga pale ambapo wana mpira ulikuwa mzuri (rest defense) idadi nzuri ya wachezaji walikuwa wanabaki nyuma

Nakupa sababu kwanini Gamondi aliamua back 3 wengi wanaweza kuamini ni kwasababu ya kujilinda sana la hasha bali kuwasogeza juu wapigaji krosi (Yao na Farid) kwasababu mshambuliaji wake (Guede) ni box straika zaidi, na pia anajua si Aziz, Pacome, Maxi ambao wanaweza kucheza pembeni kwa ufanisi na kupiga krosi na kwa wakati huo huo kuwatumia wachezaji wake hatari karibu na goli (Pacome na Aziz) kwenye muundo wa 3-4-2-1 na 5-3-2 bila mpira .

Kitu pekee ambacho Yanga mara kadhaa walikuwa wanajipiga risasi mguuni ni kama ifuatavyo:-

1: Wachezaji wengi walikuwa wanataka kuwa shujaa wa kuamua mechi badala ya kufanya Yanga kuwa shujaa: sehemu ya kupasia, kurahisisha jambo wana complicate sana.

2: Kukosa umakini, utulivu (sloppy in possession) mipira inatupwa kirahisi sana. Nafikiri Yao anaongoza kwa kuwa mtulivu zaidi uwanjani zaidi ya wenzake.

3: Ni kama kulikuwa na presha kubwa ya kushinda mechi mapema.

NOTE

1: Kagera wana golikipa mzuri, footwork, anatawala eneo lake vizuri

2: Hakuna kitu Minziro atataka zaidi kwa wachezaji wake, wamejituma sana

3: Pasi ya Aziz, Movement ya Mudathir na umaliziaji wake ni class.

4: Maxi anahitajika kutuliza sana akili katika nyakati sahihi

5: Yao, huyu haitaji tena maelezo

6: Timu zimegoma kupishana na Yanga sasa hivi

FT: Yanga 1-0 Kagera.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live