Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Timu za soka zafungana 95-0, 91-1, uchunguzi wafanyika

We Are Pumped For The Super Eagles Match Sierra Leones Bakayoko Timu za soka zafungana 95-0, 91-1, uchunguzi wafanyika

Wed, 6 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Matokeo yasio ya kawaida ya mechi mbili za soka timu za Daraja la Kwanza ambazo zimezalisha jumla ya magoli 187 yanafanyiwa uchunguzi na Shirikisho la Soka la Sierra Leone (SFLA).

Mechi hiyo iliyopigwa juzi Julai 4, 2022, Kahunla Rangers imeifunga Lumbenbu United magoli 95-0 huku Gulf FC ikishinda 91-1 dhidi ya Koquima Lebanon.

Kabla ya mechi hizo, Kahunla na Gulf FC zilikuwa pointi sawa na ziliwania nafasi ya kusonga mbele kupanda daraja.

Kilichoshangaza ni kuwa hadi mapumziko katika michezo hiyo iliyochezwa muda sawa, matokeo yalikuwa 2-0 na 7-1, hivyo kipindi cha pili ndipo mvua ya mabao ikaanza.

SLFA imesema haiwezi kuvumilia upangaji wa matokeo tena wa wazi huku ikieleza kuwa uchunguzi utafanywa kwa waamuzi wote, viongozi wa timu zote, wachezaji wa timu zote nne na yeyote atakayekisiwa kuwa alihusika katika kupanga matokeo ili sharia ichukue mkondo wake.

Matokeo hayo ya jumla ya mabao 187 huenda yakawa yamevunja rekodi ya mabao mengi zaidi kuwahi kufungwa kwenye historia ya mchezo wa soka ndani ya dakika 90.

Inatajwa kuwa, mabao mengi zaidi kuwahi kufungwa kwenye mechi moja ndani ya dakika 90 ni mwaka 2002 nchini Madagascar ambapo AS Adema iliichapa SO l'Emyrne kwa jumla ya bao 149-0.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live