Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Timu za Algeria hazitamani kucheza na timu za Bongo

Taifa Algeria.jpeg Timu za Algeria hazitamani kucheza na timu za Bongo

Tue, 12 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mtangazaji wa masuala ya soka kutoka Clouds Media, Alex Luambano amesema kuwa Timu za Algeria hazitamani tena kukutana na timu za Tanzania.

Hii inakuja ikiwa ni siku chache baada ya Timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' kufuzu fainali za AFCON 2023 kwa kutoa sare na Timu ya Taifa ya Algeria.

Ikumbukwe pia kuwa, mwezi Juni, Klabu ya Yanga ilicheza fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika na Klabu ya USM Alger ya nchini humo na kufungwa nyumbani huku ikienda kushinda ugenini nchini Algeria.

"Nilipokuwa Algeria kwa ajili ya mechi ya Algeria vs Tanzania, niliwauliza mashabiki kadhaa kuhusiana na ushiriki wa klabu zetu kwenye mashindano ya CAF [Ligi ya Mabingwa na Kombe la Shirikisho].

"Msimu uliopita Yanga ilicheza Fainali ya Kombe la Shirikisho la CAF dhidi ya USM Alger ya Algeria, Simba ilicheza Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Wydad Casablanca.

"Waliniambia kuwa, klabu za Algeria hazitamani tena kukutana na klabu za Tanzania, lakini zamani walikuwa hadi wanatengeneza mazingira ya kupangwa na klabu za Tanzania.

"Sasa hivi klabu za Tanzania zimekuwa sio salama tena kwao kuja kupita na kwenda hatua inayofata!," amesema Alex Luambano.

"Sijaenda kufanya surgery ya kutengeneza dimpoz, utaratibu wa kupata dimpoz kama hizi unaweza ukaufanya hata nyumbani kwako," amesema Zari.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live