Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Timu yetu inasemwa mbovu ila wachezaji wetu wanagombewa - Ahmed Ally

Ahmed Ally Xxx Timu yetu inasemwa mbovu ila wachezaji wetu wanagombewa - Ahmed Ally

Fri, 3 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Meneja wa habari na Mawasiliano na Simba SC, Ahmed Ally amesema klabu yao inasemwa kuwa ni mbovu lakini wachezaji wake wanaongozwa kwa kutakiwa na vilabu vingine.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Ahmed ameweka picha ya Kibu Denis akiwa na wachezaji wenzake wa Simba na kushusha ujumbe huo.

"Licha ya timu yetu kusemekana ni mbovu lakini ndio timu inayoongoza kwa wachezaji wake kuhitajika na vilabu vingi zaidi vya ndani na nje nchi

Ni dhahiri kuwa tuna kikosi chenye Wachezaji bora

Hatujapata matokeo mazuri msimu huu lakini haindoi ukweli kuwa wachezaji wetu ni bora sana ndio maana wanatajwa sana sokoni

Tunachoenda kukifanya hivi sasa ni kubaki na wale bora wenye moyo wa kuitumikia Simba

Katika dirisha hili la usajili tunaemtaka atabaki Simba lengo ni kutengeneza Simba tishio turudi kwenye Ufalme wetu."

Chanzo: www.tanzaniaweb.live