Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Timu yapata bao baada ya miaka miwili

Skysports San Marino Euro Timu yapata bao baada ya miaka miwili

Fri, 20 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Unaambiwa kwa mara ya kwanza ndani ya miaka miwili, timu ya taifa ya San Marino imefunga bao kwenye michuano rasmi, licha ya kupoteza mabao 2-1 dhidi ya Denmark kwenye mchezo wa kufuzu Euro uliopigwa usiku wa leo.

Mshambuliaji wa Manchester United, Rasmus Hojlund, ndiye aliyeifungia Denmark timu iliyofuzu nusu fainali ya Euro 2020.

Lakini Alessandro Golinucci alisawazisha katika dakika ya 61, na kuamsha shangwe kali kutoka kwa mashabiki wa Marino.

‘Minnows’ San Marino hawakuweza kushikilia bomba, dakika ya 70 Yussuf Poulsen aliipa ushindi wa bao la pili Denmark na kufuzu Euro 2024.

San Marino sasa wamepoteza mechi 83 kati ya 84 za kufuzu Euro, isipokuwa sare tasa dhidi ya Estonia mwaka 2014.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live