Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Timu ya masoko ya Azam yapata ajali

Azam Ajali D Timu ya masoko ya Azam yapata ajali

Fri, 17 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Timu ya idara ya masoko na mauzo ya Azam FC, imepata ajali alfajiri ya leo katika eneo la Magunike Dumila mkoani Morogoro, ilipokuwa safarini kuelekea Mwanza ambapo vijana hao wa mitaa ya Chamazi watacheza mchezo wa nusu fainali ya #CRDBBankFederationCup dhidi ya Coastal Union.

Kwa mujibu wa taarifa ya Azam FC, ndani ya gari hilo binafsi kulikuwa na watu watatu, Meneja wa idara, Tunga Ally na wasaidizi wake wawili, Ayubu Shelukindo na Venock Mkisi.

Meneja Tunga Ally aliyekuwa akiendesha, ndiye aliyeathirika lakini wengine waliobaki walitoka salama.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live