Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Timu ya Nyumbu yapiga mbili za kirafiki, yatoka 1-1 na Mashujaa

Nyumbu (600 X 342) Timu ya Nyumbu yapiga mbili za kirafiki, yatoka 1-1 na Mashujaa

Thu, 28 Sep 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Timu ya soka ya Nyumbu ya mkoani Pwani inayojiandaa na Ligi Daraja la Pili imetoka sare ya bao 1-1 dhidi ya timu ya Polisi Tanzania kwenye mchezo wa kirafiki uliofanyika Uwanja wa Chuo cha Polisi Kurasini jijini Dar es Salaam.

Timu ya Nyumbu huo ni mchezo wake wa pili wa kujipima nguvu uliochezwa jana Jumatano ukitanguliwa na uliochezwa juzi Jumanne na timu ya Mashujaa ya mkoani Kigoma inashiriki ligi Kuu Tanzania Bara na kutoka sare ya 1-1 kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Baada ya michezo hiyo, Kocha Mkuu wa timu hiyo, Rajab Gwamku alisema anafurahishwa na viwango vya wachezaji wake kupitia michezo hiyo ya kujipima nguvu waliocheza.

Gwamku alisema wataendelea kucheza michezo ya kirafiki zaidi ili kuiimarisha timu yake kabla ya kuanza kwa michezo ya ligi daraja la pili kwa kipindi itakapopangwa kuchezwa ligi hiyo.

Aliwaomba wanapwani kuiunga mkono timu yao ili iweze kufanya vyema kwenye ligi daraja la pili na kupanda daraja la kwanza huku malengo yakiwa ni kupanda ligi kuu ili kuuwakilisha vyema mkoa huo.

Alisema michezo yote waliocheza ilikuwa mizuri kwao kwani wao wanaenda kuboresha sehemu ambazo walikuwa hawajafuzu vizuri ili watakapoingia katika kucheza ligi waweze kupanda daraja.

"Mchezo ulikuwa mzuri timu ya Mashujaa na Polisi Fc imeweza kutupa nguvu za kucheza vizuri zaidi mbeleni katika mechi tulizocheza nazo za kirafikiki," alisema

Alisema katika timu zote wameweza kutoka sare hivyo inaonesha ni namna gani sasa wameanza kufuzu mchezo huo na kuwa tayari kuingia ulingoni katika kupata kuhakikisha wanapata ligi.

Naye Kocha wa Mashujaa, Hussein Bunu alisema katika mechi yao ya kirafiki waliyocheza na Nyumbu ilikwenda vizuri kwani imewafanya kufanya mazoezi ya kwenda katika mechi zijazo na kuwa tayari katika kufanya vizuri.

"Tumecheza vizuri na tumepata mazoezi ya kufanyia kazi katika mechi zijazo zinazokuja za ligi msimu huu," alisema

Alisema timu ya Nyumbu kuelekea msimu wao mpya wa ligi daraja la pili, timu hiyo ipo vizuri kwani wamewapa kitu ambacho wao wataenda kukifanyia kazi katika mechi zao zijazo.

Chanzo: Mwanaspoti