Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Timu ya Gadiel Michael yashuka daraja PSL

Gadiel Michael South Timu ya Gadiel Michael yashuka daraja PSL

Wed, 15 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Timu ya Cape Town Spurs anayoichezea Mtanzania Gadiel Michael Kamagi imeshuka daraja Ligi Kuu ya Afrika Kusini (PSL).

Cape Town wameshuka wakiwa sebuleni wakiangalia mechi ya Orlando Pirates dhidi ya Richards Bay ambapo Richards Bay walishinda kwa bao 1-0.

Kikanuni, timu ya mkiani PSL hushuka moja kwa moja, na ya juu yake hupata nafasi ya pili kucheza play off.

Katika michezo miwili iliyosalia, hata kama Cape Town Spurs watashinda michezo yote hawataweza kuzifikia alama 27 za Richards Bay, hivyo kukosa nafasi ya play off.

Cape Town Spurs inanolewa na Kocha Ernst Middendorp aliyewahi kuifundisha Singida Fountain Gate, ambaye ndiye aliyemsajili Gadiel Michael Spurs.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live