Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Timu tatu hazitashikika EPL

Man City Watwaa Ubingwa Uingereza Kwa Mara Ya Nne Mfululizo Man City

Sun, 11 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha wa Bayer Leverkusen, Xabi Alonso amesema Arsenal, Manchester City na Liverpool ni kati ya timu ambazo zitasumbua sana kwenye Ligi Kuu England kwa msimu ujao.

Alonso ambaye alikutana na Arsenal wakati timu yake ilipocheza nayo mchezo wa kirafiki na kupoteza kwa mabao 4-1, anaamini hakutakuwa na mabadiliko makubwa sana katika msimamo wa ligi kwa msimu ujao ukilinganisha na ilivyokuwa msimu uliopita.

Arsenal ambayo msimu uliopita ilimaliza katika nafasi ya pili nyuma ya Manchester iliyochukua ubingwa, inatafuta ubingwa wake wa kwanza wa ligi tangu msimu wa 2003/04.

Kwa msimu uliopita Liverpool, Arsenal na Man City zote zilikuwa na nafasi kubwa ya kuchukua ubingwa kabla ya mambo kubadilika dakika za mwisho na Man City kunyanyua ndoo kwa tofauti ya pointi mbili dhidi ya Arsenal.

“Arsenal sio tu mwaka jana wamekuwa na timu nzuri inayoendelea kutengenezwa chini ya Mikel Arteta ambaye amefanikiwa kutengeneza wachezaji bora kwenye timu kubwa, watatoa changamoto kubwa katika vita ya kuwania ubingwa, ninaona wataungana pamoja na Man City na Liverpool na baadhi ya timu nyingine.”

Kocha wa Arsenal, Mikel Arteta bado anaamini timu yake inahitaji kuendelea kuwa bora kwani bado haijafikia kule ambako yeye anahitaji wafike.

“Tuna mambo mengi bado ya kujifunza, tunaweza kuwa bora zaidi ya hapa kwa siku za usoni.”

Man City kwa sasa ndio bingwa mtetezi wa taji hilo ikilichukua mara nne mfululizo huku msimu uliopita ikilinyakua kwa tofauti ya pointi mbili mbele ya vijana wa washika mitutu wa Arteta.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live