Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Timu pekee zenye uhakika wa kubaki Ligi Kuu

Yanga X Coastal Uhakika Timu pekee zenye uhakika wa kubaki Ligi Kuu

Sat, 11 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ukitazama msimamo wa Ligi baada ya mechi za juma lililopita, ni Yanga, Azam, Simba na Coastal Union ndio ambazo zimejihakikishia kubaki kwenye Ligi kwa ajili ya msimu ujao!

Kuanzia nafasi ya tano [5] ambayo inashikiliwa na Tanzania Prisons yenye alama 33 sawa na KMC, alama hizo zinaweza kufikiwa na timu za chini kabisa kwenye msimamo! Ni Mtibwa Sugar pekee ndio hawezi kufikisha alama 33, ikishinda mechi zake zote zilizobaki itafikisha alama 32.

Tabora United ambayo ipo nafasi ya pili kutoka mwisho [15] kama itashinda mechi zake zote zilizobaki itafikisha alama 35, Geita Gold ambayo ipo nafasi ya 14 ikishinda mechi zake zote [4] itafikisha alama 36 wakati Mashujaa iliyopo nafasi ya 13 ikishinda mechi zote itafikisha alama 38.

Timu inayoshika nafasi ya tano [Tanzania Prisons] ina alama 33, huku timu 14 zimebakiza michezo minne [4] kumaliza Ligi, Simba na Dodoma Jiji zimebakiza michezo mitano [5] kumaliza Ligi, timu inayoshika nafasi ya pili kutoka mwisho inafasi ya kufikisha alama 35!

Maana yake ni kwamba Ligi bado mbichi! Kimahesabu bingwa bado hajatajangazwa japo Yanga ipo kwenye nafasi nzuri sana ya kutwaa ubingwa lakini hadi sasa bado hakuna timu iliyoshuka daraja.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: