Wed, 15 Mar 2023
Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Mechi ya Bournemouth na Liverpool zilipokutana kwenye Ligi Kuu England, Jumamosi iliyopita ilikutanisha timu mbili ambazo zilikuwa hazijapewa Penati tangu kuanza kwa msimu huu 2022/23.
Lakini, Liverpool walipata tuta kwenye mechi hiyo na Mohamed Salah akakosa na hivyo kuwafanya Bournemouth kuwa ni timu pekee ambayo haijawahi kupewa penalti kwenye Ligi Kuu England msimu huu.
Ligi Kuu ya England kwa sasa ipo mzunguko wa 27 huku zikiwa zimebaki mechi 11 kumalizika kwa msimu.
Je, Bournemouth watamaliza msimu pasipo kupata Penati?
Chanzo: www.tanzaniaweb.live