Droo ya hatua ya Makundi ya Ligi ya Mabingwa ya CAF ya TotalEnergies CAF na TotalEnergies Confederation Cup itafanyika Ijumaa, 06 Oktoba 2023 jijini Johannesburg, Afrika Kusini. Droo itaanza saa 12h00 GMT (14h00 Johannesburg).
Kwa mara ya kwanza kwenye historia ya CAF Champions League, Tanzania itakuwa na timu mbili kwa wakati mmoja kwenye Droo ambayo itafanyika Africa ya Kusini kuanzia saa tisa Alasiri.
Yanga wanarejea Group Stage ya CAF Champions League kwa mara ya kwanza baada miaka 25.
Kwa Simba wao ni kama nyumbani, kkatika misimu 6 wameingia group stage mara 4. Na mara ya mwisho ni miezi 6 tu iliyopita.
Mataifa ya Misiri na Tunisia yanaungana na Tanzania kwa kuingiza timu mbili mbili kwenye Group Stage. Al Ahly, Pyramid, Esperance na Etoile Du Sahel.
Bingwa mtetezi ni Al Ahly ambaye alichukua ubingwa wake wa 11 Kwa kumfunga Wydad Casablanca 3-2 kwenye matokeo ya Jumla.
Timu zote 16 zitagawanywa kwenye vyungu 4 tofauti tofauti. Kila timu itaomba kutokutana na timu nyingi kutoka chungu cha kwanza ambazo ni Al Ahly, Wydad Casablanca, Mamelodi Sundown na Esperance lakini lazima kila timu ikutane na mmoja kati ya hawa wakubwa.
Kila timu pia itaomba kutopangwa na timu kutoka Kaskazini ambao ndo ukanda wenye mafanikio zaidi ya kisoka ingawa litakuwa jambo gumu kwa sababu ya ukanda huo kuwa na timu kwenye vyungu vyote.
Stori kubwa nyingine ni Jwaneng Galaxy ya Botswana ambao wamewatoa mabingwa wa Mwaka 1995 Orlando Pirates ya Africa ya Kusini kwa mikwaju ya penati . Nouadhibou ya Mauritania wamewatoa Real Bamako ya Mali.
Kuna uwezekano mkubwa tu wa Kariakoo DERBY. Kama vipi CAF watuletee kuna kitu nataka nione.
Hizi ni timu 10 ambazo zimewahi kushirki mara nyingi zaidi kwenye hatua ya Makundi ya CAFCL.