Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Timu England zakabana koo saini ya Tammy Abraham

Tammy Abraham Return Tammy Abraham

Sun, 16 Jun 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Everton imeungana na Tottenham, Aston Villa na West Ham kwenye vita ya kuiwania saini ya mshambuliaji wa AS Roma, Tammy Abraham, 26, dirisha hili.

Tammy ambaye msimu uliomalizika alifunga bao moja, anataka kurudi England baada ya kila siku mambo kuendelea kuwa magumu kwenye kikosi cha Roma. Mkataba wake unamalizika mwaka 2026.

Inaelezwa Roma inahitaji walau Pauni 20 milioni kwa ajili ya kumuuza fundi huyu dirisha hili kiasi ambacho timu zote zinazomhitaji zipo tayari kutoa.

Kwa sasa vita iliyopo ni kwenye masuala ya masilahi binafsi kwa mchezaji na timu itakayoweka ofa kubwa ya mshahara ndiyo inampata.

Tammy anapokea mshahara wa Euro 110,962 kwa wiki na ofa anayohitaji inaelezwa ni mara mbili ya mshahara huo.

Alitua Roma akitokea Chelsea na kiwango chake bora kilimfanya ahusishwe na miamba mingi Ulaya kabla ya kuamua kuendelea kusalia Italia na sasa anatamani kurudi kucheza England mahali amabako palilitangaza jina lake.

MABOSI wa Arsenal wamepanga kukubali ofa yoyote kuanzia Pauni 30 milioni na kuendelea kutoka timu itakayohitaji saini ya kiungo wao Emile Smith Rowe dirisha hili. Rowe mwenye umri wa miaka 23, msimu uliopita hakupata nafasi kubwa ya kucheza katika kikosi cha kwanza cha washika mitutu hao. Mkataba wake unamalizika mwaka 2026. Msimu uliomalzika alicheza mechi 19.

WINGA wa Arsenal, Reiss Nelson, 24, amewasilisha barua kwa mabosi wa washika mitutu hao na kuwaambia anataka kufahamishwa juu ya uwezekano wa kupata nafasi ya kucheza kwenye kikosi cha kwanza msimu ujao ama aondoke dirisha hili. Nelson ambaye msimu uliomalizika amecheza mechi 24 za michuano yote, mkataba wake unatarajiwa kumalizika mwaka 2027.

CHELSEA imepewa ruhusa na mabosi wa Aston Villa kuzungumza na mshambuliaji wao Jhon Duran kuhusu masilahi binafsi kabla ya kurudi kwao kujadili ada ya uhamisho. Staa huyu wa kimataifa wa Colombia amekuwa kwenye rada za Chelsea tangu mwezi uliopita. Tangu atue Villa katika dirisha la majira ya baridi mwaka jana, amecheza mechi tatu tu za Ligi Kuu England.

ASTON Villa imetuma maombi ya kutaka kumsajili beki wa kushoto wa Chelsea, Ian Maatsen ambaye msimu uliopita alicheza kwa mkopo Borussia Dortmund. Maatsen mwenye umri wa miaka 22, anahusishwa kutaka kuendelea kusalia Dortmund ambayo ipo tayari kumnunua au kumchukua tena kwa mkopo wa msimu mmoja. Mkataba wa fundi huyu unamalizika mwaka 2026.

CHELSEA inaishawishi Crystal Palace kukubali kumuuza winga wao Michael Olise dirisha hili kwa kiasi kisichozidi Pauni 60, milioni. Olise mwenye umri wa miaka 22, mkataba wake unamalizika mwaka 2027, na Chelsea ina matumaini makubwa wao ndio watakamilisha mchakato wa kumsajili fundi huyu ambaye wameshafikia makubaliano naye binafsi.

MANCHESTER United inataka kugeukia mabeki wengine baada ya kuona kuna ugumu kwa Everton kukubali kumuuza Jarrad Branthwaite dirisha hili. Licha ya mazungumzo ya muda mrefu, Everton inaripotiwa kuendelea kushikilia msimamo wa kutaka kiasi kikubwa cha pesa tofauti na kile Man United inachohitaji kukilipa na kuna uwezekana Man United ikaongeza pesa ili kumpata.

BEKI wa West Ham, Kurt Zouma, 29, anatarajia kukutana na kocha mpya wa timu hiyo, Julen Lopetegui kujadili ikiwa anamhitaji ama aondoke dirisha hili. Zouma ambaye msimu uliomalizika alicheza mechi 33 za michuano yote, mkataba wake unamalizika mwaka 2025. Licha ya kuonyesha kiwango bora chini ya kocha aliyepita David Moyes, inaelezwa kocha mpya Julen Lopetegui hana mpango naye.

Chanzo: Mwanaspoti