Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Timu 17 kuwania ufalme wa soka mkoa wa Arusha

Football 2 Timu 17 kuwania ufalme wa soka mkoa wa Arusha

Thu, 1 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jumla ya timu 17 zinatarajia kuchuana vikali katika mashindano ya Ligi ya mkoa wa Arusha yanayotarajia kuanza Jumamosi Septemba 3 mwaka huu katika viwanja mbalimbali.

Akizungumzia mashindano hayo, Katibu Msaidizi wa Chama cha Soka mkoa wa Arusha, Gabriel Anthony amesema kuwa maandalizi yote ya mashindano yamekamilika huku akitoa onyo kali kwa timu zinakatojitoa ufahamu wa kukiuka kanuni za soka.

"Mashindano yanakwenda msimu Jumamosi, sisi kama chama tumefanya yetu, nitumie nafasi hii kuzikumbusha klabu shiriki makubaliano ya vikao na taratibu tulizojiweke juu ya kufuata taratibu, Sheria na kanuni za Mashindano" alisema Anthony na kuongeza....

"Hakika hatutakuwa tiyari kufumbia macho timu zitakazojaribu kuharibu taswira ya Mashindano hayo kwa vurugu au aina yoyote Ile ya utovu wa nidham, wajue kabisa adhabu zilizoko kwenye Sheria na kanuni za mpira zitachukua mkondo wake" alisema katibu huyo.

Akizitaja timu shiriki na makundi yao, Anthony alisema kuwa kundi A, lina jumla ya timu sita ambazo Ascona, Sumawe, Beach boys, Scorpion, Bodaboda fc na Monduli fc.

"Kundi B' Lina timu sita pia ambazo ni Olasiti, Domingo, Arusha city, Royal, Nyota na Meserani huku kundi C' kukiwa na timu Tano tu ambazo ni Kakakuona, USA Star, Kilinga, Future star na Csc fc"

Alisema baada ya hatua ya awali, vinara wawili wa Kila kundi, watacheza hatua ya sita Bora itakayofanikisha bingwa kupatikana huku Kila timu iliyoshika mkia katika kundi lake kushuka daraja hadi wilayani.

Katika Mashindano hayo, timu ya Bodaboda fc itafungua pazia rasmi dhidi ya wageni wao Sumawe fc mtanange utakaopigwa katika uwanja wa Karatu.

 Huku Monduli Coffee fc wakiwakaribisha wageni wao Ascona fc katika uwanja wa Monduli mechi zote zikipigwa majira ya saa 10 jioni.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live