Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Timo Werner arejea RB Leipzig

Timo Werner Return Timo Werner

Tue, 9 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Straika wa Ujerumani Timo Werner anajinadaa kurudi katika klabu yake ya zamani baada ya klabu ya Chelsea na RB Leipzig kufikia makubaliano ya kitita cha pauni milioni 25.

Timo atatua Leipzig siku ya Jumanner kwaajili ya kufanyiwa vipimo ili kukamilshwa kwa dili hiyo ambapo baadaye utafanyika mchakato wa mkataba.

Werner ambaye ametimiza miaka 26 alichangia katika mabao 44 Chelsea kwenye michezo 89 tangu alipoijiunga na The Blues mwaka 2020 kabla ya kutua darajani alikuwa akiichezea Leipzig ambako alifunga mabao 95 katika michezo 159.

Licha ya Juventus kuonesha nia ya kutaka kumsajili, Werner anataka kurejea katika klabu yake ya zamani ya RB Leipzig ili kujiweka sawa kwa ajili ya Kombe la Dunia litakaloanza Novemba

Werner anayetarajiwa kuwasili Ujerumani wiki hii, hakuwepo kwenye kikosi cha Chelsea kilichopata ushindi dhidi ya Everton Jumamosi iliyopita kwenye mchezo wa Premier League.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live