Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tiketi Gumzo Fainali za Kombe la Dunia 2022

Skysports Football Qatar World Cup 5422462 Tiketi Kombe la Dunia 2022 kufuru

Thu, 10 Feb 2022 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Wakati ikibaki miezi tisa kabla ya fainali za Kombe la Dunia mwaka huu kuanza huko Qatar, jumla ya mashabiki milioni 17 wametuma maombi ya kununua tiketi za kutazama mechi za mashindano hayo.

Idadi hiyo ya mashabiki imerekodiwa katika awamu ya kwanza ya mauzo ya tiketi ambayo ilianza Januari 19 hadi Februari 7 mwaka huu.

Taarifa iliyotolewa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA), imeonyesha kuwa idadi kubwa ya maombi ya tiketi ni kwa ajili ya mchezo wa fainali wa mashindano hayo.

Jumla ya watu 1.8 milioni wametuma maombi ya tiketi kwa ajili ya kutazama mechi ya fainali itakayochezwa kwenye Uwanja wa Lusail, Disemba 18.

Idadi kubwa ya mashabiki waliotuma maombi ya tiketi ni wale wanaoishi nchini Qatar wakifuatiwa na wengine kutoka mataifa ya Ulaya, Amerika Kusini na Amerika Kaskazini.

Ukiondoa maombi kutoka Qatar, nchi nyingine ambazo mashabiki wake wametuma idadi kubwa ya maombi ya tiketi za kutazama fainali hizo ni Argentina, Brazil, England, Ufaransa, India, Mexico, Saudi Arabia, Falme za Kiarabu na Marekani.

Fainali za Kombe la Dunia zitashirikisha jumla ya timu za taifa 32 kutoka mabara mbalimbali ambazo zitagawanywa katika makundi nane yenye timu nne kila moja.

Hadi sasa jumla ya timu 15 zimeshafuzu fainali hizo za Kombe la Dunia 2022 zikisubiri nyingine 17.

Timu hizo 15 zilizofuzu ni Qatar, Ujerumani, Denmark, Ufaransa, Brazil, Ubelgiji, Croatia, Hispania, Serbia na England.

Nyingine ni Switzerland, Uholanzi, Argentina, Iran na Korea Kusini.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz