Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tigere arudi Zimbabwe

Tigereee Tigere arudi Zimbabwe

Tue, 30 Jan 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Aliekuwa kiungo wa Ihefu, Mzimbabwe Never Tigere (33) amerejea nchini kwao baada ya mkataba kumalizika na kujiunga na Ngezi Platinumz inayoshiriki Ligi Kuu nchini humo.

Uhamisho huo umetamatisha safari ya kiungo huyo kwenye Ligi Kuu Bara aliyoianza miaka minne iliyopita alipojiunga na Azam FC akitokea FC Platinum ya nchini kwao na baadaye kutua Ihefu.

Akizungumza kwa njia ya simu kutoka Zimbabwe, Tigere alisema ulikuwa ni wakati mzuri kucheza Ligi ya Tanzania na sasa anaenda kuitumikia Ngezi Platinumz.

“Nitarudi Tanzania. Ni nchi nzuri na yenye watu wakarimu sana. Nimecheza hapo nikiwa na Azam na baadaye Ihefu, zote ni timu nzuri lakini kwa sasa naelekeza nguvu zangu katika timu yangu mpya,” alisema Tigere ambaye alisifika kwa kupiga vyema mipira ya kutenga ‘faulo’ na msimu huu ameifungia Ihefu mabao mawili.

Chanzo: Mwanaspoti