Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Thomas Tuchel asema hatashawishiwa na mashabiki kusalia Bayern Munich

Thomas Tuchel Asema Hatashawishiwa Na Mashabiki Kusalia Bayern Munich Thomas Tuchel asema hatashawishiwa na mashabiki kusalia Bayern Munich

Sat, 27 Apr 2024 Chanzo: Bbc

Mkufunzi wa Bayern Munich Thomas Tuchel anasema hatakubali "kushawishiwa" na ombi la kumtaka abaki katika klabu hiyo.

Ombi la kumtaka kocha huyo mwenye umri wa miaka 50 kusalia Allianz Arena limetiwa saini na zaidi ya mashabiki 12,000.

Bayern ilitangaza mwezi Februari kwamba Tuchel ataondoka katika klabu hiyo mwishoni mwa msimu huu, mwaka mmoja kabla ya mkataba wake kumalizika.

"Ingawa mada hii ni nzuri kwangu wakati [mashabiki] wanataka ubaki, sio jambo la kipaumbele," alisema Tuchel.

Ralf Rangnick, kocha wa zamani wa Manchester United, amefanya mazungumzo na Bayern kuhusu kuchukua mikoba ya Tuchel msimu huu wa joto.

Tuchel aliongeza kuwa ni jukumu la klabu kumteua mrithi wake na ameziba masiko ili "kutosikia" uvumi wowote.

Chanzo: Bbc